Wolper awa mbongo kwa mtoto wake

0
120

Muigizaji wa Bongo Movie, Jackline Wolper amevunja ukimya kwa kueleza kwamba mtu yeyote ambaye atamchafua au kumdhalilisha mtoto wake atamchukulia hatua za kisheria.

Wolper mwenye weupe na uzuri wake ulioambana na umbo lenye kuvutia ,amevunja ukimya huo ambapo ameweka wazi hawezi kumjibu kila mtu mtandaoni ,hivyo sheria itachukua mkondo wake.

“Siwezi kumjibu kila mtu atakayekuwa akimdhihaki mtoto wangu bali nitatumia sheria zaidi na kwa sasa watu wawili wa mitandaoni kurasa za udaku nimewafikisha katika sheria ndio sababu ya kutoona picha zangu za ujauzito hazisambazwi zikiwa na matangazo ya kuhusu tiba za afya,” amesema.

Wolper ametumia nafasi hiyo kueleza sababu za kutomuonyesha kwa muda mrefu katika Mitandao ya kijamii kama ilivozoeleka kwa mastaa pamoja na watu mbalimbali mara baada ya kujifungua.

Wolper ambaye amepewa ubalozi katika duka la nguo Sweetrolah amesema hivi ;”Niliingia mkataba na Kampuni ya Sweetrolah tangu nilivyokua na ujauzito wa miezi tisa, nikaona niwe wa kipekee kabisa nisisambaze picha za mtoto mahali popote pale.”

LEAVE A REPLY