Wolper avutiwa na maisha ya K-Linny

0
213

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa huwa anavutiwa na K Lynn Mengi kutokana na mafanikio aliyokuwa nayo.

Wolper amesema kuwa anampenda sana K Lynn na mara nyingi amekuwa akizifuata nyayo zake ili siku moja aje kuwa kama yeye au zaidi ya yeye.

Wolper amesema kwamba mara nyingi amekuwa akimfuatilia K Lynn kwa sababu ni mwanamke mpambanaji, anajitambua na hana skendo kama ilivyo kwa watu maarufu wengine, hivyo tabia yake nzuri na nidhamu kwenye jamii ndio vinavyomfanya azidi kumpenda.

Muigizaji amesema kuwa “Huwezi amini mimi na yule dada tunafanana majina mpaka tarehe za kuzaliwa, yeye amezaliwa Desember 6, 1978 wakati mimi nimezaliwa Desember 6, 1987, nadhani ndio maana damu zetu zimepatana.

Pia amesema kuwa “Jack angekuwa na skendo za ajabuajabu sidhani kama ningemfuatilia, anajiheshimu na anafanya mambo yake kwa akili sana ndio maana namfuatilia, hivyo kati ya watu ambao wanani-inspire namba moja ni yeye natamani siku moja na mimi nije kuwa kama yeye au nimzidi kabisa,”.

LEAVE A REPLY