Wolper atamani kurudi shule baada ya Jux kuhitimu Chuo China

0
345

Muigizaji wa Bongo Movie, Jackline Wolper amempongeza mwanamuzki, Jux baada ya kuhitimu chuo nchini China.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Wolper ameandika kama ifuatavyo “nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…!

Ameongeza, “hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” amemaliza kwa kuandika.

Jux jana kupitia akaunti yake ya Instagram ameonesha picha akiwa katika mahafali yake nchini China ambapo amehitimu Degree yake ya Computer Science.

LEAVE A REPLY