Wolper amualika Hormonize kwenye ‘birthday party’ yake

0
152

Muigizaji wa Bongo movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hana wivu wa kimapenzi kwa Harmonize na mpenzi wake Sarah na ndio maana amewaalika wote wawili kwenye party ya birthaday yake.

Wolper na Harmonize waliachana miezi michache iliyopita baada ya kuwa pamoja kwa muda. Baada ya kuachana kila mmoja alimtuhumu mwenzie kwa kuchepuka huku Wolper akiweka wazi kuwa waliachana kwa sababu Harmonize alikuwa na uhusiano.

Lakini hata baada ya kuachana na kila mmoja kupata mpenzi ambapo Harmonize alianzisha uhusiano na Sarah na Wolper alianza uhusiano na Brown lakini bado wawili hao wamekuwa na bifu la chini chini.

Siku ya jana ilikuwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wolper ‘birthday’ ambapo yeye mashabiki zake pamoja na ndugu zake walienda kushiriki kula chakula cha mchana na kituo  cha kulelea watoto yatima Temeke.

Wolper aliweka wazi kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na Harmonize wala  mpenzi wake mzungu Sarah ndio maana amewaalika kwenye sherehe yake.

LEAVE A REPLY