Wolper akanusha kuwa mjamzito

0
23

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa anashangaa sana kuona watu wengi wanaisubiria mimba yake kwa hamu wakati mimba za mastaa wengine hajawahi kusikia foleni hiyo ya watu.

Wolper amewatoa hofu watu hao kwa kuwaambia, suala la mimba halijifichi kwani kama ipo haiwezi kujificha kwa sababu mimba hainywei bali inakua siku hadi siku hivyo wawe wapole tu mpaka muda utakapofika itaonekana bila kificho au kama ni mtoto, watamuona.

Amesema kuwa “Bado najiuliza maswali mengi sana kwa nini watu wanaisubiria kwa hamu mimba yangu yaani kuna kitu gani cha ziada maana kuna wasanii wengi sana kwa kipindi hiki wamepata ujauzito mbona hawakuwasubiria hivi.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Ninachoamini mimi ni kwamba mimba haijifichi hata kidogo, watulie tu kwani kama ni mimba watu wataiona”.

Wolper kwasasa yuko kwenye uhusiano na mfanyabiashara Richie Mitindo ambapo watu wanadai kuwa uhusiano huyo umanza kuzaa matunda baada ya Wolper kushika ujauzito lakini mwenyewe anapinga hilo.

LEAVE A REPLY