Wolper adai wanaume wa kuhonga magari siku hizi hakuna

0
189

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa maisha yamekuwa magumu ndiyo mana siku hizi hakuna wanaume wa kuhonga magari na pesa kama zamani.

Msanii huyo wa filamu amepost video fupi yenye dakika moja, ambayo anamuomba Mungu awarudishie wanaume hao wa zamani wenye tabia hizo.

“Nina miaka kama miwili hivi zile fujo za waya sizisikii, kama mwanaume kamnunulia gari la IST mwanamke wake basi anatokea pedeshee anamwambia mtoto mzuri kama wewe hufai kutembelea gari hilo la misaada na kupeleka watoto shule, halafu yeye anakupa Range Rover”.

Pia amesema kuwa  “Hata ukisema unakaa Sinza anakwambia uhamie Masaki, Mungu na Yesu naomba uturudishie wale wanaume wa zamani waliokuwa wanatuhonga Range Rover”.

Pia Jacqueline Wolper amekiri kwamba, amewahi kudanga kwa kuwa na mwanaume mwenye pesa ili kusaidia kuendeleza maisha yake.

LEAVE A REPLY