Wolper adai hana mpango na hela za kuongwa na wanaume

0
151

Staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa mwanamke yeyote ni vyema akajituma kwasababu hakuna mwanaume anayehonga kwasasa.

Wolper alisema kuwa, zamani mwanamke alikuwa anashindwa kujitegemea kwa sababu alijua kuna hela atapewa na mwanaume fulani, lakini kwa sasa hiyo haipo kwani wanaume nao wamebana hivyo ni bora wakajituma na kujisimamia mwenyewe kwenye kazi wanazozifanya.

Amesema kuwa “Mambo ya kusubiria hela ya kuhongwa nilishafuta kwenye kichwa changu ndipo nikapata nguvu ya kufanya kazi zangu maana hela za kuhongwa sizitaki kabisa,”.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa sasa kazi yake ya ushonaji imemfanya kuanza kujulikana hadi nje ya nchi huku akiwandaa wasichana wadogo ili waweze kujitegemea.

LEAVE A REPLY