Wizkid afuata nyayo za Beyonce, Rihanna na Kanye West

0
184

Mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid amevunja rekodi baada ya kufanikiwa kuujaza ukumbi wa O2 Arena jijini London Uingereza kwenye show yake ya AfroRepublik iliyofanyika usiku wa May 26,2018.

Wizkid alisindikizwa na mastaa mbalimbali kutokea Nigeria ambao walimpa company juu ya stage akiwemo Mr Eazi, Tiwa Savage, Tekno, Maleek Berry na wengine kibao na kuperform nyimbo zao wenyewe.

Rekodi hiyo aliyoivunja Wizkid ilishawahi kufanywa na mastaa wakubwa duniani kama Beyonce, Rihanna, Kanye West ambapo ukumbi huo wa O2 una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 20,000.

Mmoja wa mastaa wakubwa waliohudhuria show hiyo ni mwanamitindo maarufu kutokea Uingereza Naomi Campbell.

LEAVE A REPLY