Wizi wa mitihani chanzo cha kuchomwa shule za serikali – Kenya

0
184

Gazeti binafsi la Daily Nation linalochapishwa nchini Kenya limetoa ripoti mpya inayoonyesha kuwa uchomwaji moto wa majengo ya shule za sekondari nchini humo unasababishwa na ‘wizi wa mitihani’

Gazeti hilo limemnukuu waziri wa elimu, Fred Matiangi akidai kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wizi wa mitihani ya taifa unachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la uchomwaji moto wa majengo ya shule.

Kwenye mahojiano hayo, waziri Matiangi amenukuliwa akisema:

Wanafunzi wanaokabiliwa na mashtaka hayo baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi wamekiri kuhusika na wamesema sababu kubwa ya kufanya vitendo hivyo ni hasira.

Hasira hizo hutokana kulipia mitihani lakini hadi wanapoingia kufanya mitihani ya mwisho wanakuwa hawajapokea mitihani waliyoilipia’.

Zaidi ya shule za sekondari za serikali 100 zimechomwa moto nchini Kenya mwaka huu huku baadhi ya wanafunzi waliohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC wakidai kuwa huchoma moto shule zao ili kupata muda wa likizo kutokana na shughuli za masomo.

LEAVE A REPLY