Wivu wamponza Dayna Nyange

0
38

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amesema kuwa kinachomfanya aachane na wapenzi wake mara kwa mara ni wivu uliokisiri.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Homa, alieleza kwamba akimpata mpenzi, huingia mazima na kujikuta akiathiriwa na wivu.

“Mimi huwa sidumu muda mrefu na wanaume kwa sababu ya wivu, huwa namfuatilia kwa kila kitu, hapo sasa anatakiwa awe makini.

Pia amesema kuwa “Huwa nahitaji kujua yuko wapi na anafanya nini, nikiona haeleweki naumia na kuona ananiongopea, mwisho wa siku tunaachana,”.

Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva, kwasasa anafanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva kutokana na nyimbo zake kufanya vizuri.

LEAVE A REPLY