Winnie Mandela aijia juu Serikali ya Afrika Kusini

0
193

Aliyekuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ‘Winnie Madikizela Mandela’ ameishukia serikali ya nchi hiyo kuwa imeiingiza nchi kwenye janga.

Ametoa kauli hiyo katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Mandela amesema kuwa nchi hiyo imefanya kosa kubwa kwani chama tawala cha ANC  kinaharibu nchi hiyo.

Kauli ya Mama Winnie inakuja wakati ambapo kumekuwa na shinikizo la kumuondoa madarakani Rais Jacob Zuma kutokana na kashfa kubwa za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili.

Rais Zuma anakubwa na kashfa ya kujihusisha na familia tajiri ya Gupta ambayo imedaiwa kuwa na uwezo wa kuingilia teuzi mbalimbali za viongozi pamoja na maamuzi yanayofanywa na serikali.

LEAVE A REPLY