Wimbo wa Zuchu ‘Litawachoma’ waweka rekodi

0
63

Video ya wimbo wa Litawachoma wa mwanamuziki Zuchu umefikisha jumla ya watazamaji milioni nane kwa muda wa mwezi mmoja toka wimbo uachiwe.

Wimbo huo Zuchu amemshirikisha Diamond Platumz imeweka rekodi mpya kwa nyimbo zake ambazo ametoa kwa miezi ya hivi karibuni ambapo wimbo huo umefikisha watazamanji milioni nane kwa muda wa mwezi mmoja.

Rekodi hiyo iliyowekwa kwa nyimbo huyo imetoka upande wa YouTube ambapo aliuweka wimbo huo Sep 28, 2020 ambapo mpaka sasa unajumala ya watazamaji 8,104,615.

Litawachoma ni wimbo ambao umeingia katika chati mbalimbali za muziki kama vile Billboard Afrika na pia kushika nafasi ya 82 kutazamwa duniani kote kwa upande wa YouTube.

LEAVE A REPLY