Wimbo wa Lady Jay Dee wazua utata

0
24

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee ameingia kwenye hatari ya kufungiwa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘One Time’ baada ya kudaiwa kuhamasisha matumizi ya uvutaji wa bangi.

 

Hatua hiyo imekuja, baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), kuthibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa muziki, kuhusu mashairi ya wimbo huo.

 

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema baada ya kupokea malalamiko hayo, sasa wanaendelea kufanya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na nini hasa dhumuni la mstari huo kwenye hiyo nyimbo.

 

“Tumeliona hilo na suala hili lipo kwenye position ya kufanyiwa kazi, baada ya kuifuatilia. Kwa hiyo, niishie kusema tu kwamba, tunaendelea kulishughulikia jambo hili baada ya kufanya uchunguzi,”

 

Wimbo huo ambao Jide aliuachia Septemba 14, mwaka huu, unaripotiwa na wadau mbalimbali wa burudani kuwa, maudhui yake yanaonyesha kuhamasisha matumizi ya bangi.

 

Ndani ya wimbo huo, moja ya mistari yake unasema “Tusmoke weed one time” mstari uliozua utata, hasa kwa wadau wengi wakisema unakiuka maadili.

LEAVE A REPLY