Wimbo wa Lady Jay Dee ‘One Time’ wafungiwa

0
41

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wametoa maamuzi ya kuufungia wimbo wa ‘one time’ ya Komando Lady Jaydee kwa kosa la kuhamasisha vitu visivyokuwa na maadili na nchi ya Tanzania.

Meneja wa msanii huyo Mx Carter amesema kuwa siku ya leo wamepokea barua rasmi ya kufungiwa kwa wimbo huo kwenye vituo vya Radio, TV na mitandaoni.

Pia amesema kuwa “Tuliitwa kwa sababu kuna vitu wao kama BASATA waliona havijakaa sawa, tukaitikia wito kwa Lady Jaydee kwenda ili kuzungumza nao, na leo tukapokea barua rasmi ya kuamua kuufungia na hautoruhusiwa kupigwa kwenye vituo vya Radio TV na kwenye mitandao kama wa YouTube”.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Kuna mstari ambao nisingependa kuutaja ila wanasema unahamasisha vitu ambavyo sio maadili ya kitanzania.

LEAVE A REPLY