Wimbo wa Harmonize ‘Kwangwaru’ wafungiwa nchini Kenya

0
117

Wimbo wa Kwangwaru wa wasanii wa WCB, Diamond Platnumz na Harmonize umefungiwa kuchezwa kwenye mashule nchini Kenya kutokana na wimbo huo kukosa maadili.

Wimbo huo unapendwa na kuchezwa sana nchini Kenya umefungiwa kutokana na kuwa na maudhui yenye matusi.

Mkurugenzi wa (KFCB) Ezekiel Mutua amesema serikali imefungia muziki na maonesho yote kutoka nje ya Kenya ambayo yanaenda kinyume na sharia utu na utamaduni wa Kenya

“Mashindano na disco lazima ziwekewe vikwazo ili kuhakikisha wasanii wa kigeni hawatoruhusiwa kuja Kenya na kuharibu maadili, tamaduni na mila yetu. Kwa nini wanafanya muziki ambao wamepigwa marufuku katika nchi zao kwenda Kenya? “Aliuliza Mutua.

Aidha, Mutua anasema KFCB itashirikiana na serikali za mitaa, wizara ya mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa ili kuhakikisha kanuni zinatekelezwa.

“Watu wanaomualika Diamond na watu wengine kufanya maonesho hapa na hata maudhui ambayo yamefungiwa Tanzania na nchi nyingine yoyote. Kuzuia mchakato wa kukimbia kodi kwa sababu unapofanya mkataba na mwanamuziki huyo na kuiweka pesa moja kwa moja unakataa kodi za serikali. Hiyo ni rushwa, “aliongeza Mr Mutua.

Afisa huyo alisema watoto wadogo wanapaswa kulindwa kutokana na maudhui yaliyofichika katika baadhi ya nyimbo za wasanii.

LEAVE A REPLY