Wimbo wa Harmonize ‘Ushamba’ yaweka rekodi

0
161

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameweka rekodi baada ya wimbo wake mpya Ushamba kufikisha watazamaji milioni 2 ndani ya masaa 48 katika mtandao wa Youtube.

Kupitia wimbo wake mpya wa Ushamba, Harmonize amefikia rekodi iliyowekwa na kushikiliwa kwa muda mrefu na Wimbo wa Seduce Me wa Alikiba kwenye Mtandao wa YouTube.

Wimbo huo wa Ushamba umeweka rekodi ya kusikilizwa na kutazamwa mara zaidi ya milioni 2 ndani ya saa 48. Rekodi kama hiyo iliwekwa na Wimbo wa Seduce Me mwaka 2017.

Kwa upande wake, Wimbo wa Ushamba umevunja rekodi ya video zote za wasanii nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa kusikilizwa na kutazamwa mara nyingi zaidi ndani ya saa 48.

Video hiyo ambayo iliachiwa rasmi Novemba 8, mwaka huu, imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya video zote zinazotrendi Tanzania na Kenya.

Rekodi nyingine ambayo pia imevunjwa na Wimbo wa Ushamba ni ile iliyowekwa na video ya Wimbo wa Salome wa msanii Diamond Platnumz akishirikiana na Rayvanny ambao ulitazamwa mara zaidi ya milioni moja ndani ya saa 48.

Kuna kila dalili kuwa Wimbo wa Ushamba ukaendelea kupata watazamaji wengi zaidi kutokana na jinsi unavyoendelea kutazamwa kwa kasi.

LEAVE A REPLY