Wimbo wa Despacito waweka rekodi

0
35

Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Dady Yankee umeifikia namba ambayo haijawahi kufikiwa kwenye mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watu wengi kuliko nyimbo yoyote dunia.

Ngoma hiyo imefikisha jumla ya watazamaji BILIONI 7 kwenye mtandao wa YouTube hivyo kuweka rekodi ya kuwa video iliyotazamwa zaidi kwenye historia ya mtandao huo.

Tafiti zinasema kwa idadi hiyo ya VIEWS, ni kama kila binadamu hapa ulimwenguni ameitazama video hiyo kwani dunia ina jumla ya watu Bilioni 7.8 kwa takwimu za mwaka 2020.

Mbali na ‘Despacito’ kuweka rekodi hiyo ya muda wote, namba mbili inashikiliwa na video ya Baby Shark Dance – Pinkfong Song yenye jumla ya VIEWS Bilioni 6.8, Ed Sheeran – Shape of You kwenye nafasi ya tatu ikiwa na VIEWS Bilioni 5.01.

See You Again ya Wiz Khalifa VIEWS Bilioni 4.7 na Top 5 inafungwa na katuni ya Masha And The Bear – Recipe for disaster yenye VIEWS Bilioni 4.3.

LEAVE A REPLY