Wimbo wa Alikiba yaanza kufanya vizuri youtube

0
164

Baada ya video ya wimbo ‘Mvumo wa Radi’ ya Ali Kiba kufanyiwa figisu figisu katika mtandao wa youtube hatimaye video hiyo sasa yarejea kwa kishindo mtandaoni.

Inavyosemakana kuwa akaunti ya mwanamuziki huyo ilidukua na watu wasiojulikana na kusababisha views kutokuongezeka katika akaunti yake ya YouTube.

Video hiyo ilikaa zaidi ya saa 20 huku idadi ya walioitazama ikiwa inapanda na kushuka tofauti na wimbo wake wa Seduce Me.

Kwa upande wa Alikiba amesema kuwa anachoridhika nacho hivi sasa ni jinsi ambavyo watu wanavyoendelea kufurahia muziki wake mzuri hata kama views hazionekani YouTube.

 Pia Kiba amesema kuwa menejimenti yake ilifanya mawasiliano ya moja kwa moja na YouTube kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

Kwasasa tatizo hilo limekwisha na imefikisha views 1.1 milioni hadi leo sasa katika akaunti yake youtube.

LEAVE A REPLY