Whozu avamiwa na kutishiwa bastola kisa Tunda

0
252

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Whozu amefunguka na kuweka wazi kuwa alinyolewa nywele na kutishiwa kupigwa risasi na aliyekuwa mpenzi wa mrembo Tunda aitwaye Ali.

Mkasa huo umetokea baada ya mwanaume huyo kuwakuta Whozu na Tunda wakiwa chumbani kwa mrembo huyo jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo ameeleza kuwa alianza uhusiano na Tunda baada ya kumueleza kuwa ameachana na mpenzi wake.

Pia Whozu amesema kuwa kabla ya kupata kauli hiyo ya Tunda, alikuwa ameshapigana na huyo jamaa mjini Moshi kutokana na ugomvi ulioibuka kwa sababu ya wivu wa mapenzi.

Ameeleza kuwa Februari 25 mwaka huu alikuwa nyumbani kwa mrembo huyo maeneo ya Mbezi, ambapo akiwa na rafiki zake ‘Wabantu’ ambao walienda kwa ajili ya kuangalia filamu, walikaa hadi usiku wa manani na wakaamua kulala.

Whozu ameendelea kueleza kuwa yeye alilala na Tunda chumbani lakini ghafla nyumba hiyo ilivamiwa na watu wapatao sita ambao waliruka ukuta, wakavunja mlango hadi wa chumbani na kuwapiga wote waliokuwa ndani.

Ameeleza kuwa wakati akijaribu kujitetea kwa kupigana na watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga na marungu, hasimu wake huyo alitoa bastola na kumuelekezea kichwani akitishia kumpiga risasi.

Amedai baada ya kutulia, mtu huyo alimtaka mmoja kati ya wenzake waliovamia kumkata nywele, na ndipo amri hiyo ilipotekelezwa wakati yeye akiwa mpole akihofia kupigwa risasi.

Msanii huyo ameeleza kuwa aliripoti tukio hilo polisi ambapo alipewa ushirikiano wa kutosha, hivyo anaamini sheria itachukua mkondo wake.

LEAVE A REPLY