Wenger aitoa Arsenal ‘big four’ msimu huu

0
176

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa klabu hiyo haiwezi kushika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kutokana na matokeo wanayoyapata.

Wenger ambaye ni raia wa Ufaransa amesema kuwa timu hiyo imeshika nafasi nne bora na kufuzu kombe la klabu bingwa kwa miaka 20 iliopita.

Lakini ikiwa imesalia mechi 10, Arsenal iko katika nafasi ya sita ikiwa ni nyuma ya timu nne zinaozoongoza ligi hiyo.

”Ni changamoto kubwa kuwa katika nafasi nne bora lakini nadhani inawezekana”, alisema Wenger.

”Nimeweza kufanikiwa kwa miaka 20 iliopita na ilikuwa vigumu. Sasa imekuwa muhimu so nafurahia kwamba watu wamegundua sio rahisi kama inavyoonekana”.

Mwaka 2012 Wenger alisema kuwa miongoni mwa nafasi nne bora ni sawa na kushinda taji na maoni hayo yaliungwa mkono na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola.

LEAVE A REPLY