Wema Sepetu kumleta Van Vicker Bongo

0
349

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa ataleta msanii wa filamu kutoka Ghana, Van Vicker kuhudhuria sherehe yake ambayo itaambatana na uzinduzi wa filamu.

Wema amesema Van Vicker atawasili saa 10 alfajiri hapo kesho na kulakiwa na watu mbali mbali akiwemo yeye mwenyewe, na kisha kumpeleka kupumzika yakifuatiwa na mandalizi ya tukio kubwa la uzinduzi wa filamu yao walioigiza pamoja, Day After Death, ambalo anakusudia kulifanya siku ya tar 28, Septemba.

“Well kama nilivyoandika Van Vicjer atawasili na ndege ya kesho alfajiri, tutaenda kumpokea tukiwa na watu mbali mbali pamoja na waandishi wa habari, kisha tutampeleka hoteli kupumzika na baadaye tutakuwa na ziara kwenye vituo tofauti tofauti vya habari”, amesema Wema Sepetu.

Licha ya hayo siku hiyo pia ambayo ataadhimsha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, itahudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar es salam, Paul Makonda.

Hii ni mara ya pili kwa Wema Sepetu kumleta msanii mkubwa wa filamu kutoka nchi za Afrika Magharibi, kwani alishawahi kumleta msanii wa Nigeria Omotola Jalade Ekeinde kwenye uzinduzi wa filamu yake Super Star ambayo mpaka sasa haijaingia sokoni.

LEAVE A REPLY