Wema Sepetu hana wasiwasi kwenye mapishi

0
139

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema hana wasiwasi kwenye kumridhisha mwanaume atakaye kuwa mumewe katika kipengele cha mapishi kwani yupo vizuri.

 

Wema ambaye amefanya makubwa kunako anga la Bongo Muvi, alisema kuwa kitu ambacho anajivunia kutoka kwa mama yake ni kwamba, alimfundisha jinsi ya kupika kila kitu kama mwanamke.

 

“Kwa kweli mimi najua wanaume wengi wanapenda sana msosi, sasa mimi hakuna msosi ambao unanishinda kupika au vitafunwa vyovyote.

 

Wema amesema sasa mwanaume akinioa labda aniache kwa sababu nyingine tu na si kwamba mambo ya jikoni, niko vizuri,” alisema Wema.

LEAVE A REPLY