Wema Sepetu aweka wazi uhusiano wake na Diana Kimaro

0
532

Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa yeye atabaki kuwa dada wa msanii mwenzake Diana Kimaro na si vinginevyo.

Wema amesema kuwa atasimama kama dada kama anavyofanya kwa wadogo zake wengine katika tasnia na nje ya tasnia na ameshapunguza baadhi ya marafiki wasiofaa.

Amesema “Mimi nitabaki kuwa dada kwa Diana kama nilivyo kwa Allu au Lulu, wote wale wadogo zangu hakuna kingine”,.

Akizungumzia uhusiano wake na mama yake amesema kuwa, mama yake kukasirika ni kawaida na kama mama akichukizwa na mwanaye anatakiwa kuwa hivyo lakini wako sawa.

Hayo yanajiri baada ya mama mzazi wa mwanadada huyo kumzuia urafiki na muigizaji mwenzake Diana Kimaro kwakile alichodai kuwa urafiki wao hauna faida.

LEAVE A REPLY