Wema Sepetu awaweka fans wake roho juu kwa ‘ubuyu’

2
1353

Staa wa Bongo Movie na mlimbwende wa zamani wa Tanzania, Wema Isack Sepetu huenda akawa ndiye staa wa kike ndani ya Bongo aliyewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mastaa wa Bongo waliofanikiwa zaidi kwenye tasnia ya Burudani.

Licha ya ukweli kuwa sio sifa nzuri kwa msanii au binadamu wa kawaida kusifiwa kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi ambayo mara kwa mara hayadumu lakini huenda Wema akawa ndiye msanii anayeongoza kwa hilo kwa upande wa mastaa.

Siku ya jana, staa huyo kupitia akaunti yake ya Instagram alieleza mpango wake wa ‘kumwaga mchele kwenye kuku wengi’ na ikiaminiwa kuwa hivi sasa anataka kutoa majibu ya skendo ya kimapenzi inayomuandama kuhusu mpenzi waliyeachana, Idris Sultan.

Wema na Idris ambao uhusiano wao ulivuma sana kabla ya kutokea kwa ‘ajali’ ya kupoteza watoto mapacha ‘kwa mujibu wa kauli ya Idris’ kufuatia kuharibika kwa iliyokuwa mimba ya staa huyo (Wema).

Kauli hiyo ya Wema imeanza kuzua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii huku kukiwa na tetesi kuwa kitendo cha staa huyo kujiweka karibu na familia ya mpenzi wake wa zamani, Diamond platnumz ni njia ya kujirudisha taratibu kwa Dangote.

Post ya Wema kwenye mtandao wa Inasomeka hivi:

‘Kuna muda mtu unaweza ukakaa na ukasema na moyo wako, ila moyo mara nyingi huwa unazidi nguvu nyingine zozote.

‘Kuna kitu kiukweli ninacho kwa moyo wangu’

‘Lakini siwezi kusema leo wala kesho, but ipo siku isiyo na jina wala tarehe, nitakisema tu, maana mnanijua kukalfisha nafsi huwa sipendi, but all in all tuseme Inshallah,”

Je, Wema yuko mbioni kumwaga ‘ukweli wa jambo gani?’

Je, mhanga wa kauli ya Wema atakuwa nani?

Je, ‘kukalfisha nafsi’ ni kupi hasa kwa mtazamo wa Wema?

IshiKistaa itakuletea kile ambacho Wema atakiweka hadharani kuhusu kauli hiyo.

2 COMMENTS

  1. Comment: Yap Inapendeza Sana Unapo Kaa Nakujihoji Mwenye Kwa Kina Zaid Kuwa Kunamtu From Your Heart Unaempenda Damdam

LEAVE A REPLY