Wema Sepetu ampa pole Zari kufuatia kifo cha mazazi mwenzake

0
349

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amempa pole Zari The Bosy Lady baada ya kufiwa na mazazi mwenzake, Ivan Semwanga.

Wema ameonesha kuguswa na kifo hicho cha Ivan Semwanga aliyefariki usiku wa jana akiwa hospitali nchini Afrika Kusini.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Wema ametoa pole kwa familia ya Ivan pamoja na Zari ambaye amezaa nae watoto watatu wa kiume.

Wema Sepetu amesema ameumizwa na taarifa hizo huku akiwaonea huruma watoto wake ambao amewaacha wakiwa wadogo na kumfariji mama yao ambaye ni Zari.

Wema Sepetu kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Broken hearted Rest In Peace Ivan SHOCKING NEWS kwakweli… My Condolences to The whole PFamily… Mungu awatie nguvu wale watoto jamani… They are too young… And Mungu amtie nguvu Mama watoto wako… It will be a very hard period of time for all of you But it shall pass”,ameandika Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Ivan Semwanga amefariki jana usiku kwa maradhi ya Shambulio la Moyo na ameacha watoto watatu wote wa kiume.

LEAVE A REPLY