Video: Wema Sepetu ameihadaa CHADEMA au ameisaliti CCM?

0
1073

Baada ya Wema Sepetu kukutwa na uthibitisho wa matumizi ya dawa za kulevya kisha kufunguliwa kesi mahakamani, staa huyo aliibua mapya baada ya kuvuja kwa sauti yake akikosoa utaratibu uliotumika kuwakamata mastaa na kuhusisha mambo binafsi kwenye msala huo, mapya yamezuka tena.

Hivi karibuni ilipatikana tena sauti ya staa wa Bongo Movie, Steve Nyerere akiwa kwenye mazungumzo na mama mzazi wa Wema Sepetu wakijadiliana mipango mbalimbali kuhusiana na Wema kunufaika kwa kutumia skendo hiyo.

Yasikilize mazungumzo hayo yaliyorekodiwa kabla Wema Sepetu na mama yake kuhamia chama cha CHADEMA kwa madai ya kutelekezwa na CCM huku sauti hizo zikiweka wazi kuwa huo ni mpango maalum unaosukwa na wasanii kwaajili ya Wema kunufaika kifedha, yeye na familia yake.

Sauti nyingine inapatikana kwenye link hii:

https://www.youtube.com/watch?v=3ftPXfIBc7o

LEAVE A REPLY