Wema Sepetu alivyomsapoti Lema kwenye mkutano Arusha jana

2
408

Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu jana ameungana na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye mkutano na wananchi wa jimbo hilo.

Wema Sepetu amehudhuria mkutano huo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huyo baada ya kutoka gerezani alipokaa kwa miezi minne kutokana na kesi ya uchochezi ambapo alikamatwa mkoani Dodoma.

Muigizaji huyo kwasasa amejikita zaidi kwenye siasa baada ya kuhamia Chadema akitokea CCM mwezi uliopita.

Kwenye Mkutano huo Lema alielezea jinsi alivyoishi maisha ya jela kwa miezi minne pamoja  na mateso wanayoyapata wafungwa ndani ya gereza la Kisongo.

Mkutano huo ulifanyika jana na kuhuhuriwa na viongozi wa Chadema wa mkoa huo ambapo ulijaza umati wa watu wa jiji la Arusha.

 

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY