Wema Sepetu akanusha kuolewa na Diamond Platnumz

0
94

Muigizaji wa Bongo Movies, Wema Sepetu ameweka wazi kuwa yeye si mwanamke atakayeolewa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kama taarifa zinavyosambaa mtandaoni.

 

Kauli ya Wema imekuja baada ya siku za hivi karibuni Diamond kutangaza kuwa, yupo tayari kufunga ndoa ifi kapo Oktoba 2, mwaka huu.

Wema amesema kuwa, yeye na Diamondi ni watu waliobaki kuwa marafi ki tu wa karibu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao kwa sababu kila mmoja ana uhusiano wake mwingine wa kimapenzi.

 

Wema amesema kuwa kwasasa Diamond ni mshikaji wake na si vinginevyo, wala watu wasiichukulie kihivyo kwasababu yupo kwenye mahusiano na mwanaume mwingine.

LEAVE A REPLY