Wema Sepetu akanusha kumtusi Zari

0
43

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amekanusha taarifa kuwa ameungana na Tanasha Donna na Hamisa Mobeto kumtukana Zari The Boss Lady.

Wema amesema kuwa, hakuna kitu kama hicho na wala hana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa yeye sasa hivi ana mahusiano mengine na wala hana tofauti yoyote kati yake na Zari ambaye ni mzazi mwenza wa Diamond Platnumz.

Wema ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz amesema kuwa “Sijaungana na mtu yeyote kumtusi mtu na sina sababu ya kufanya hivyo.

Pia amesem“Hakuna mtu yupo kwa ajili ya kumshambulia mtu wala hakuna mtu ameungana kumshambulia mtu,”

Hivi karibuni kumeibuka mashambulizi ya vijembe kati ya Tanasha na Zari, wote wakiwa ni wazazi wenza wa Diamond ambao kwasasa wote wan je ya Tanzania.

LEAVE A REPLY