Wema Sepetu akanusha kukatwa utumbo

0
137

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na na kusema kuwa kuwa hajakonda kwajili ya kukatwa utumbo kama inavyodaiwa bali amekonda kwa ajili ya mawazo.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni muigizaji huyo kuonekana kupungua mwili wake tofauti na hapo hawali hivyo watu kuanza kutilia mashaka afya yake.

Wema kwa mara ya kwanza aliweka ‘plain’ kuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

Wema ameongeza kwa kusema kwamba, licha ya kupungua anaufurahia muonekano wake mpya kwani kuwa mnene zaidi nayo siyo poa.

Muigizaji huyo kwasasa ana kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kwa kosa la kusambaza video za utupu katika mtandao wa kijamii.

LEAVE A REPLY