Wema Sepetu akanusha kukatwa utumbo

0
110

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa muigizaji huyo alikwenda India kwa ajili ya kukata utumbo.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya watu kuhisi hayo kutokana na kupungua mwili kila siku kiasi kwamba mashabiki zae wamekuwa wakipata wasiwasi na afya yamsanii wao.

Wema amesema kuwa kitu kikubwa kilichomfanya kwenda nje ni kwa ajili ya kuangaika swala lake la kupata mtoto na hata alipoenda huku aliambiwa kuwa anatakiwa kupunguza mafuta ili aweze kupata  mtoto.

Wema amesema kuwa kinachomfanya akonde kila siku ni stress za hapa na pale lakini pia amekuwa akinywa dawa ambazo zinamsaidia kupunguza uzito  na kupunguza mafuta pia.

Muigizaji amesema kuwa ameshangazwa na baadhi ya mashabiki hao katika mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amekatwa utumbo ndiyo mana amepungua mwili tofauti na hapo awali.

 

 

LEAVE A REPLY