Wema Sepetu afunguka kutolewa mahali na wanaume wa tano

0
455

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa wanaume wa tano walijitokeza nyumbani kwao kumtolea mahali ili wamuoe lakini aliwakataa wote.

Wema amedai kuwa kuna muda wanaume watano tofauti walienda kutoa posa kwao lakini aliwakataa wote.

Walijitokeza karibu wanaume watano wanaenda, kwa mama kupeleka barua kinachotokea mama ananiita, ananiuliza mimi, sikubali kwa sababu siwezi kuolewa na mtu ambaye simjui au sijakaa naye“.

Lakini kuhusu Kuolewa hivi sasa Wema amejibu hawezi kuweka wazi lakini ana mpenzi wake ambaye anampenda lakini hawezi kumuweka wazi kwani amekuwa mtu mzima siku hizi.

Wema amefunguka na kumpongeza msanii wa Bongo fleva ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Ali Kiba kwa kufunga ndoa hivi karibuni.

LEAVE A REPLY