Wema Sepetu achaguliwa kuwania tuzo nchini Marekani

0
23

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ametajwa miongoni mwa mastaa wanaowania tuzo za Hollywood And African Prestigious Awards nchini Marekani mwaka 2020.

Wema anayefanya vizuri kwenye uigizaji ametajwa kwenye kinyang’anyiro cha utoaji wa tuzo zitakazofanyika mwaka huu nchini Marekani.

Wema, ameingia kwenye tuzo hizo akiwania kipengele cha Mwigizaji Bora wa kike wa Tamthilia za Kiafrika kupitia tamthilia yake, Karma inayoruka kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo, DSTV.

Pia Christian Bella kwenye kipengele cha Msanii Huru wa Kiume wa Kimataifa huku Zari The Boss Lady akitarajiwa kuwa mshereheshaji mdogo (Co Host) wa hafla hiyo.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 18, mwaka huu nchini Marekani na kushirikisha wasanii maarufu duniani kote kutokana na ubora wa kazi za wasanii hao.

LEAVE A REPLY