Wema Sepetu abariki Diamond kumuoa Zari

0
255

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ameshangaza watu wengi baada ya kufunguka kuwa yupo tayari kushudia ndoa ya Diamond Platnumz na Zarinah The Boss Lady.

Wema alifunguka hayo baada ya video ya wimbo wa Iyena wa Diamond ambapo ndani yake yupo Zari kama video queen ambapo ndani ya video hiyo wanafunga ndoa.

Wema alimtaka Diamond kufanya kweli na kumuoa mama watoto wake huyo ambapo aliandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Kupitia akaunti yake Instagram Wema Sepetu ameandika “New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli”.

Pia amengeza kwa kuandika “Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri”.

Zari aliweka wazi kuwa aliachana na Diamond baada ya video kusambaa zilizomuonyesha Diamond Platnumz na Wema wakikumbatiana Kwenye kumbi za starehe Miezi minne iliyopita.

LEAVE A REPLY