Wema ndani ya Arusha kumliwaza Godbless Lema. Siasa au Movie?

0
659

Staa wa filamu za Bongo na kamanda mpya wa CHADEMA, Wema Sepetu ameamua kujitolea kwenda kumtembelea kamanda mwingine wa chama hicho, Godbles Lema ambaye ameachiwa kwa dhamana.

Wema aliyekitosa chama tawala kwa madai ya kutomlipa fedha zake za kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 amesema kuwa ameamua kwenda kujifunza mengi kutoka kwa mwanasiasa huyo wa upinzani na mbunge wa Arusha.

Hata hivyo haijajulikana kama mbio hizi za staa huyo zitaishia ukingoni kama zilivyokuwa mbio za wasanii wengine wa filamu waliokuwa makamanda mwanzoni mwa kampeni za mwaka 2015 kabla ya kugeuka na kujiunga na CCM muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu.

Kwenye ukurasa wake wa INSTAGRAM Wema aliandika:

‘Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho i’ll be in Arusha kuonyesha Solidarity “FOR TO BE FREE IS NOT MERELY TO CAST OFF ONE’s CHAINS, BUT TO LIVE IN A WAY THAT RESPECTS AND ENHANCES THE FREEDOM OF OTHERS” – NELSON MANDELA #CallMeKamanda’

LEAVE A REPLY