Wema afunguka sababu ya kutohudhuria uzinduzi wa filamu ya Aunt Ezekiel

0
112

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka sababu ya kushindwa kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya ‘MAMA’ ya Aunt Ezekiel.

Uzinduzi wa filamu hiyo fupi ya dakika 20 ilifanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Wema amesema kuwa ameshindwa kuhudhuria kwenye uzinduzi huyo kutokana na kucheleweshwa na mama yake mzazi.

Ameandika  “I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie na Bovie Fleva walihudhuria kwenye uzinduzi wa filamu fupi ya ijulikanayo kama ‘MAMA’ ambapo Aunt Ezekiel ameigiza na mtoto wake Cook aliyezaa na dansa wa Diamond, Mose Iyobo.

LEAVE A REPLY