Wellu Sengo kumzalia mtoto mwingine Steve Nyerere

0
470

Muigizaji wa Bongo Movie, Wellu Sengo ambaye ali­zaa na mchekeshaji Steve Nyerere amedai kuwa anatarajia kuonge­za mtoto mwingine na mzazi mwenziye huyo.

Wellu alisema amefurahi kuwa mama na anap­enda sana watoto hivyo anategemea kuongeza mtoto mwingine na Steve Nyerere kwani ana malengo ya kuzaa watoto wanne.

“Kwa jinsi nnavyo­tamani na kupenda watoto nitaongeza mtoto mwingine soon na malengo yangu ni kupata watoto wanne hivyo namuomba Mungu anikamilishie malengo yangu,” alisema Wellu.

Muigizaji huyo ambaye ameingia kwenye uhusiano na muigizaji mwenzake ambapo kwasasa wamebalikiwa kupata mtoto wa kike.

Kwa upande wa Steve Nyerere yeye akuongelea chochote kuhusu suala la muigizaji huyo kuongeza mtoto wa pili.

LEAVE A REPLY