WCB waweka wazi kufanya kazi na Rich Mavoko

0
94

Uongozi wa WCB umesema kuwa milango yote iko wazi kwa msanii Rich mavoko kufanya show katika show zao zinazozunguka kila mkoa kwa sasa hivi inayojulikana kama wasafi festival tour.

Mmoja wa mameneja wa WCB, Babu Tale amesema kuwa hawana kinyongo chochote na msanii Rich Mavoko hata kama hapo katikati kulitokea kutokulewana.

Babu Tale amesema kuwa linapokuja suala la kufanya kazi na mwanamuziki huyo hakuna shida kwani wao nia yao kukuza muziki wa Tanzania na siyo kuwa tofauti na wanamuziki wengine.

Babu Tale amesema kuwa kwa sababu rich mavoko alishafanya show  za tigo fiesta hivyo karibia mikoa mingi anayopita kwa sasa alishapita hapo awali lakini kama wangemuwahi mapema basi ilikuwa haina haja ya kuancha kumuweka katika listi.

Babu takle anasema kuwa kwa mwaka huu acha ipite lakini kwa mwaka ujao tamasha hili litakuwa kubwa zaidi na litaongeza mikoa na pia wasanii wataongezea zaidi na watamuwahi Rich Mavoko.

LEAVE A REPLY