Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ajiuzuru

0
454

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa zao.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika kashfa kwenye Ripoti za Uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite.

Uamuzi a viongozi hao umekuja baada ya Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya usalama.

Kwa upande wake, akiongea leo Alhamisi mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.

LEAVE A REPLY