Waziri wa fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan afutiwa mashtaka ya rushwa

0
96

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali nchini Afrika Kusini ameamua kufuta mashtaka aliyomfungulia waziri wa fedha wa nchi hiyo Pravin Gordhan.

Waziri huyo wa fedha aliwahi kunukuliwa akidai kuwa mashtaka hayo hayakuwa na msingi wowote na yalifunguliwa ‘kisiasa’.

Habari za kufunguliwa mashtaka kwa waziri huyo zilisababisha kuanguka kwa biashara nchini humo na kusababisha thamani ya fedha ya nchi hiyo, Randi kushika kwenye soko la fedha la kimataifa kwa 3%.

Waziri huyo ameonekana akiwa na msimamo dhidi ya rais Jacob Zuma na baraza lake la mawaziri na amekuwa akiwaonya dhidi ya rushwa na ubadhirifu.

Kesi iliyokuwa ikimkabili inahusiana na malipo yaliyofanywa kwa wakurugenzi wakubwa wa mamlaka ya huduma za mapato ya nchi hiyo (Sars) walipokuwa wanaacha kazi wakati huo Sars ikiwa chini ya Gordhan yapata miaka 10 iliyopita.

Baada ya kupitia mashtaka, mkuu wa mamlaka ya uendeshaji mashtaka ya Afrika Kusini (NPA), Shaun Abrahams alidai kuwa hakukuwa na kusudio la jinai.

LEAVE A REPLY