Waziri wa Fedha aridhishwa na utendaji wa TRA

0
197

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameeleza kuridhishwa na utendaji wa Shirika la Reli nchini (TRL) na kusema kuwa serikali inaendelea na mpango wake wa kuimarisha reli hiyo ili iweze kuleta tija kwa uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania.

Dk Mpango amesema kwa sasa TRL inafanya kazi zake kwa ufanisi kwa kuwepo na usafiri wakati wote lakini pia kuwa na makusanyo ya kutosha ya mapato ya serikali katika mizigo na abiria.

Pia waziri huyo amemsifia mkurugenzi wa TRL, Masanja Kadogosa kwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kulinyanyua kimapato shirika hilo kwa kazi ambayo ameianza vizuri na serikali iko mbioni kujenga reli mpya ya kisasa.

Waziri huyo aliongeza kwa kusema ujenzi huo pamoja na ubunifu wa mkurugenzi huyo litaifanya reli hiyo kufanya kazi kwa tija na kutimiza lengo la serikali la reli hiyo kuwa kiungo muhimu katika kuinua uchumi wa nchi.

LEAVE A REPLY