Waziri wa Afya wa Tunisia afariki baada ya kushiriki mbio za hisani

0
85

Waziri wa Afya nchini Tunisia, Slim Chaker amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo baada ya kushiriki katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa saratani.

Slim Chaker aliugua baada ya kukimbia mita 500, kufariki kwenye hospitali ya kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya afya.

Waziri mkuu Youssef Chahed amesema kuwa amempoteza ndugu ambaye alikuwa akitoa huduma ya kibinadamu.

Mbio hizo ziliandaliwa kwenye mji wa pwani wa Nabeul siku ya Jumapili kuchangisha fedha za kujenga zahanati ya watoto ya kutibu ugonjwa wa saratani.

Chaker aliteuliwa kuwa waziri wa afya mwezi uliopita wakati wa mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.

LEAVE A REPLY