Waziri Sonyo afariki dunia

0
118

Mwanamuziki wa dansi nchini Tanzania, “Waziri Sonyo” amefariki dunia siku ya jana baada ya kutoka kutazama mechi ya Simba na Al Ahly.

Taarifa zinasema chanzo cha kifo chake ni kupanda kwa presha ya ghafla wakati anarudi nyumbani baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.

Sonyo alitamba zaidi na bendi za Chuchu Sound, TOT, African Revolution–Tam Tam na Victoria Sound amefikwa na umauti, Kibaha alipokuwa akiishi.

Taratibu za mazishi zinafanywa na ndugu zake ila kwa sasa msiba upo nyumbani kwake Kibaha Mailimoja.

LEAVE A REPLY