Waziri Nchemba aagiza kufanyika uchunguzi wa mauaji ya kiongozi wa Chadema

0
113

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Daniel John ambaye alikuwa ni Katibu wa kata ya Hananasifu (Chadema) yaliyotokea Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Waziri Mwigulu amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

“Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,” alisema Waziri Mwigulu.

Ameongeza kusema kuwa maswala ya demokrasia huamukiwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki.

LEAVE A REPLY