Waziri Mwijage: Serikali inatafuta wawekezaji wa kujenga nyumba Dodoma

0
152

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Serikali ipo katika harakati za kuwatafuta wawekezaji ambao watawekeza katika kujenga nyumba za kutosha mkoani Dodoma ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa na nyumba za kutosha kwa watumiashi wa serikali ambao wanahamia mkoani humo.

Waziri huyo amesema hatua zimeanza kuchukuliwa na wizara hiyo yenye jukumu la kutafuta wawekezaji nchini katika sekta mbalimbali hali ambayo itasaidia taifa kuongeza mapato yake kupitia tozo mbalimbali.

 

Pia amesema kwamba wameanza utekelezaji wa kutafuta wawekezaji hao ili kuja kujenga nyumba laki moja Tanzania na matarajio yao ni kujenga nyumba nyingi zaidi na ofisi yake inaunga mkono wazo la Rais la kuhamia Dodoma na kuendelea kutafuta wawekezaji wengi zaidi hasa kwa mkoa wa Dododma.

 

Vile vile Waziri Mwijage ameongeza kuwa sambamba na hilo wameanza mazungumzo na wazalishaji wa viwanda vya saruji kutoka China ambao watazalisha tani milioni saba kwa mwaka mkoani Tanga hivyo ni fursa moja wapo kibiashara nchini.

LEAVE A REPLY