Waziri mkuu wa UK, Theresa May kukutana na waziri mkuu wa Jamhuri ya Ireland

0
162

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May anatarajia kukutana na kufanya kikao na waziri mkuu wa Ireland, Enda Kenny ambacho kinachotarajiwa kutawaliwa na ajenda ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Ireland atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea waziri May kwenye ofisi zake zilizopo kwenye mtaa wa Downing baada ya Bi. May kuteuliwa kushika wadhifa wa waziri mkuu.

Wawili hao wanatarajiwa kujikita kwenye ajenda zinazohusu mipaka na hali ya uchumi kutokana na uamuzi wa kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya.

Bunge la chama cha wafanyakazi wa Uingereza limeitaka serikali yao kushughulikia masuala ya uchumi na usalama ndani ya muungano wan chi zinazounda UK kabla ya kusonga mbele na kuendela na majadiliano ya kujitoa EU.

Tayari Bi. May ameshaweka wazi kuwa Uingereza inahitaji muda kujiandaa ikiwemo kupanga mikakati ya kiuchumi na kujadiliana na viongozi wa chini, wafanya biashara na viwanda kujiandaa na miaka kadhaa inayotarajiwa kuwa migumu ya mapatano.

Tayari Bi. May ameshafanya vikao na viongozi wenye ushawishi mkubwa kwenye EU, kansela Angela Merkel wa Ujerumani na rais wa Ufaransa, Francois Hollande.

LEAVE A REPLY