Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May kuzuru Ujerumani na Ufaransa

0
211

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Theresa May ameanza rasmi majukumu ya kiti hicho kipya kwa ziara ya Ujerumani ili kukutana na kansela wan chi hiyo Angela Merkel hii leo kujadiliana juu ya uamuzi wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili kukamilisha zoezi hilo.

Mazungumzo kuhusu Brexit yanatarajia kutawala mlo wa usiku wa wawili hao huku May akitarajia kukuza ufahamu wake na uhusiano na kiongozi mwenzake wa Ujerumani.

Ziara hiyo ya Ujerumani inatarajiwa kufuatiwa na ziara ya nchini Ufaransa ambapo Bi. May anatarajia kukutana na rais wa nchi hiyo Francois Hollande.

‘Nimedhamiria kuona Uingereza inafanikiwa katika kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya na hiyo ndio sababu nimeamua kutembelea Ujerumani na Ufaransa muda mfupi tangu nitwae madaraka ya uwaziri mkuu’. Amesema Bi. May

‘Ziara hizi zitakuwa fursa muhimu ya kuimarisha uhusiano wa kiutendaji ambao natarajia kuupata kwa viongozi wengi zaidi kwenye Umoja wa Ulaya kwenye kipindi cha wiki kadhaa au miezi ijayo’. Ameongeza Bi. May

Kwenye mazungumzo yake na viongozi hao wenye nguvu na ushawishi mkubwa kwenye Umoja wa Ulaya, waziri May anatarajia kurudia tena kauli yake ya kuwataka viongozi wa Ulaya waipe muda Uingereza ili iweze kuzungumza Uskochi, Wales na Ireland Kaskazini ili kufikia muafaka wa kujitoa.

Bi. May ameshamwambia rais wa baraza la Ulaya, Donald Tusk kuwa nchi yake haitochukua mamlaka ya urais wa baraza hilo mwaka 2017 kama ilivyokuwa imepangwa tangu awali.

LEAVE A REPLY