Waziri mkuu wa Ufaransa azomewa na waombolezaji

0
136

 

Baadhi ya wananchi wenye hasira wa Ufaransa wamemzomea waziri mkuu wa nchi hiyo Manuel Valls na kumwita jina la muuaji na kumtaka ajiuzuru wadhifa huo.

Kelele za watu hao zilikuja wakati wa maombolezo ya mauaji ya watu 84 waliouawa kwa kukanyagwa na loli siku ya Alhamisi kabla ya kuanza kwa sala ya dakika moja iliyofanyika nchi nzima.

Mapema kabla ya tukio hilo rais
wa zamani wa nchi hiyo na kiongozi wa zamani Nicolas Sarkozy aliishutumu serikali ya rais Hollande kwa kushindwa kuwalinda wananchi wan chi hiyo.

Serikali ya Ufaransa inaendelea kupeleka askari kwenye maeneo ya watalii kuchunguza uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano wa mauaji hayo na makundi ya kigaidi.

Mpaka sasa wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa imeshindwa kupata ushahidi wa kumuunganisha muuaji Mohamed Lahouaiej Bouhlel na makundi ya kigaidi huku ikiwashikilia watu 6 ili kuwahoji.

Mtke wa Mohamed Lahouaiej Bouhlel (hawakuwa wakiishi pamoja) alikamatwa na na kuhojiwa na polisi siku ya Ijumaa na kuachiwa siku ya Jumapili.

LEAVE A REPLY