Watu wawili wamepigwa risasi Kibiti usiku wa kuamkia leo

0
259

Watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema kuwa waliofanya uhalifu huo wamewachukua majeruhi na kuondoka nao kusikojulikana.

Kamanda Lyanga amesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risasi na wahalifu kutokomea nao kusikojulikana.

Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo ambao walitajwa kuwa ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.

Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu alisema ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.

LEAVE A REPLY