Watu watano wafariki dunia nchini Kenya

0
133

Watu watano wamefariki dunia kutokana na maandamano yaliyotokea katika mji mkuu wa Nairobi wakati wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakikusanyika uwanja wa ndege kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi huyo.

Makundi ya watu yalikusanyika katika uwanja wa ndege kumkaribisha kiongozi huyo amabye alikuwa amerejea kutoka mataifa Marekani.

Raila Odinga alisusia marejeleo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Kulikuwa na ripoti za maafisa wa polisi waliorusha vitoa machozi katika gari la Raila Odinga alipokuwa akielekea mjini.

Siku ya Jumatatau Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta alibuka mshindi.

LEAVE A REPLY